Ofisa wa Ubalozi Mtanzania Afariki Dunia Kwa Ajali, Malaysia - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ofisa wa Ubalozi Mtanzania Afariki Dunia Kwa Ajali, Malaysia

Apolonia Mwangosi (46), enzi za uhai wake

Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia, Apolonia Mwangosi (46), amekufa papo hapo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutumbukia mtoni mjini Kuala Lumpar.

Mkuu wa Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani cha Ampang, Malaysia, Hambazi Abdulrahman alisema ajali hiyo ilitokea juzi karibu na mgahawa katika eneo la Ampang Waterfront Food Court.

Abdulrahman alisema katika ajali hiyo iliyotokea saa 7.30 usiku, dereva wa gari hilo, Linus Okafor (35), raia wa Nigeria alipata majeraha kidogo.

Msemaji wa familia, Hagulwa Mbogo alisema mwili wa marehemu utawasili nchini kesho kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kisiga alithibitisha kuwapo taarifa za kifo hicho na kwamba, wizara inashirikiana na ubalozi wa Malaysia na familia ya marehemu kurejesha mwili kwa maziko.

Chanzo: Mwananchi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.