Ndege ya Flydubai Yapata Ajali na Kuua Abiria Wote Huko Urusi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ndege ya Flydubai Yapata Ajali na Kuua Abiria Wote Huko Urusi

Ndege ya FlyDubai
Ndege ya FlyDubai
Ndege ya abiria imepata ajali mashariki mwa jiji la Urusi la Roston-on-Don, na kuua abiria wote 55 na wafanyakazi saba, wamesema maafisa.
FlyDubai Boeing 737-800, iliyokuwa inatoka Dubai, ilikosa barabara ya kutua wakati ilipojaribu kuua siku ya Jumamosi.
Haijafahamika nini kilichosababisha ajali hiyo ili mwanga hafifu na upepo mkali vinadaiwa kuwa chanzo.
Ndege hiyo ilipata ajali mashariki mwa jiji la Urusi la Roston-on-Don
Ndege hiyo ilipata ajali mashariki mwa jiji la Urusi la Roston-on-Don
Picha za CCTV zilionyesha mlipuko na mwanga mkali baada ya ndege kupata ajali.
“Ndege ilidondoka chini na kukatika vipande vipande,” Kamati ya Uchunguzi ya Urusi ilieleza kwenye tovuti.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.