Mzee Yussuf Afuta Akaunti za Instagram za Wake Zake, Adai Kujitoa Hivi Karibuni Pia - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mzee Yussuf Afuta Akaunti za Instagram za Wake Zake, Adai Kujitoa Hivi Karibuni Pia


Wakati wanawake duniani kote wakiadhimisha siku ya wanawake duniani jumanne hii, wake wa mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusufu, Leila Rashid na Chiku wamekatazwa kutumia tena mtandao wa Instagram.
Wanawake hao wamekatazwa kutumia mtandao huo na endapo watatumia kwa siri mume wao huyo amewaeleza kwamba ndiyo itakuwa talaka yao.

Mzee Yusufu amechukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuzuka kwa majibizano ya wake zake hao kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsap na Instagram.

Akizungumza weekend hii katika kipindi cha taarabu kinachorushwa na Radio Clouds FM, Mzee Yusufu, alisema mtandao huo ndio chanzo kikubwa cha kukuza mgogoro huo.

“Nimewatoa wake zangu wote kwenye mtandao huu ambao ndio nimeona umekuza sana mgogoro huu na mimi pia nipo njiani kutoka katika akaunti hiyo ili ibaki kwa ajili ya kazi tu na endapo nitagundua yeyote ana simu ya siri ambayo anaitumia kuingia kwenye mtandao huo ndiyo itakuwa talaka yake,” alisema.

Aliongeza, “Hivi tunavyozungumza wake zangu wote hawana akaunti za Instagram, zinazoendelea kusambaza maneno ni majina feki na ndiyo nimeshaamua hivyo,”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.