Msanii Huwezi Kufanya Kazi Peke Yako - Lady Jaydee - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Msanii Huwezi Kufanya Kazi Peke Yako - Lady Jaydee

Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva , Lady jaydee maarufu kama Komando ambaye sasa anatamba na wimbo wake mpya wa ‘Ndi Ndi ndi’ amefunguna na kuweka wazi sababu zilizomfanya kuwa chini ya uongozi na kudai kama msanii huwezi kufanya kazi kazi peke yako.

Lady Jaydee alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo alidai kuwa aliamua kuwa chini ya uongozi wa Seven Mosha sababu ni mtu ambaye anafahamiana naye kwa miaka zaidi ya kumi na tano na kusema ni mtu ambaye anapatana naye sana hivyo aliona ni bora asaidiane nae ili kuweza kufanya mambo mengine mazuri zaidi kwenye muziki.

“Unajua Seven Mosha nimemjua kwa zaidi ya miaka 18 hivyo siyo mtu mpya, lakini tunaelewana sana niliona kushirikiana nae naona tunaweza kufanya kitu kizuri zaidi, lakini pia hata kipindi cha nyuma nilikuwa nikishirikiana na baadhi ya watu katika kufanya kazi zangu” alisema Lady Jaydee.

Katua hatua nyingine Lady Jaydee alisema kuwa muziki ni mizuka hivyo ikitokea mizuka anaweza kufanya kazi na msanii Ali Kiba ambaye yupo naye chini ya menejimenti moja pia alisisitiza kuwa video ya wimbo wake huu mpya itatoka baada ya wiki mbili kuanzia leo.

Eatv.tv

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.