Mrembo Lulu Amechukua Nafasi ya Hamisa Mobeto kwa DJ Majay ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mrembo Lulu Amechukua Nafasi ya Hamisa Mobeto kwa DJ Majay ?

Kikohozi cha mapenzi kimeendelea kuyakaba makoo mengi. Baada ya Barakah Da Prince na Naj kushindwa kuzuia chao, Lulu na DJ Majay wameonekana kushindwa kukihimili chao pia.
Udaku mjini unadai kuwa mshindi wa tuzo za AMVCA 2016, Elizabeth Michael aka Lulu amechukua nafasi ya Hamisa Mobeto kwenye moyo wa CEO huyo wa EFM.

Majay alimsindikiza Lulu kwenye tuzo hizo zilizofanyika jijini Lagos, Nigeria.

Baada ya muigizaji huyo kushinda tuzo, Majay hakusita kumpongeza.
“Congratulation Madam,You Made all of us proud Keep it up! @elizabethmichaelofficial @elizabethmichaelofficial,” aliandika Majay kwenye Instagram.

Picha hiyo ilivutia comments nyingi za kufurahisha na inaonekana kuna watu walikuwa wanaujua uhusiano huo tayari.

new_husnaa: Majizo me napita kaka dancerdancer@elizabethmichaeloffic

lovie_lovie_lovie: This is the most painfull feeling to a woman. Seeing ur man with someone else. Not jus a woman. A successfull woman. Anyway congrats lulu. U made it babe gal.

elizabethmichael_fashion_icon: Tokeni povu lkn baby wa bae wangu ndo keshapongeza

hassanuraji: Penzi nikikohozi jmn ukimpenda mtu huwezi kuficha wala kujali ya watu hongera bro @majizzo@munalove100 @elizabethmichaelofficial

bellynashotz: @majizzo chukua soda nakuja kulipa

ashawaismael: Duuuu mambo kweeeupeee

tinabegere: Malipo chini ya jua hata kama si leo ipo siku. Kumbuken wenzenu pia wana mioyo ya nyama si ya chuma!

trixnicolas: Mbona watu mapovu yanawatoka.. ivi majay aliwahi kupost cheti cha ndoa na mtu?? .. hebu muacheni … shkanaa fanya yako mama.. umetumwa hela uchagani sio kuuza sura… go mama goooo… ila nimependa iyo apo juu destination…. buhahahahahahahaha

jaqy13: mungu wangu napost inaonyesha imetumwa kutoka Lagos nigeria mmmhh crycrycrycry@majizzo

Hata hivyo wengine hawajasita kwenda kumpa pole Hamisa.

officialjoyvieve: Ucjali babe, mambo ya kawaida tu ayo, deal with your doutah mungu yupo

charity_mimi: Polee mwayaa mana umemanuliaa kakumwagiaa umemzaliaa kakupiga chinii na kumpenda mwinginee inaumiza sanaa sidhani kama hata unapata usongizii

Majizzo na Hamisa walibahatika kupata mtoto wa kike, Fantasia.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.