Messi, Ronaldo Wasababisha Kifo India - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Messi, Ronaldo Wasababisha Kifo India

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Ballon d’Or mara tatu.

Mtu mmoja ameuawa baada ya kubishana na rafiki yaje juu ya nani ni mchezaji bora wa dunia kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Raia mmoja wa Nigeria Michael Chukwuma, 21, alimchoma visu mwenzake Obina Durumchukwu katika mtaa mjini Mumbai, polisi wa India walisema.

Tukio hilo lilitokea kufuatia sherehe ya Jumamosi usiku.

“Walikuwa wakijadili kuhusu wachezaji soka. Mmoja ni shabiki wa Messi, mwingine alikuwa ni wa Ronaldo,” alisema polisi mchunguzi.
Lionel Messi ameshinda tuzo Ballon d’Or mara tano

“Kuliibuka fujo wakati wa mazungumzo. Marehemu alirusha glasi usoni mwa mshtakiwa. Glasi ilipasuka na kusababisha majeraha kidogo usoni.”

“Baada ya hapo mshtakiwa alichukua glasi na kumshambulia nayo marehemu ambaye alifariki kutokana na kuvuja damu nyingi.”

Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tano, huku Cristiano Ronaldo akiondoka nayo mara tatu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.