Mbwana Samatta Aipatia Timu yake Bao la Ushindi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mbwana Samatta Aipatia Timu yake Bao la Ushindi.

WALSH (WA PILI KULIA) AKIWA NA SAMATTA PAMOJA NA WACHEZAJI WENGINE WA GENK WAKISHANGILIA USHINDI WAO DHIDI YA CLUB BRUGGE.

Beki kisiki wa KRC Genk, Sandy Walsh amempongeza Mbwana Samatta kwa bao lake la kwanza akiwa na kikosi hicho.

Walsh ametupia picha wakiwa na wachezaji wengine pamoja na Samatta katika mtandao wa kijamii wa Facebook akimpongeza Samatta baada ya kufunga bao la tatu katika mechi dhidi ya Club Brugge ikiwa ni dakika chache tu baada ya kuingia. Katika mechi hiyo, Genk iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Mtanzania huyo amejiunga na Genk akitokea mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DR Congo ambayo kwa kiasi kikubwa aliisaidia kubeba ubingwa huo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.