Matokeo ya Mechi za Klabu Bingwa Barani Ulaya March 16 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Matokeo ya Mechi za Klabu Bingwa Barani Ulaya March 16

Michuano ya klabu bingwa barani ulaya iliendelea tena March 16 kwa michezo miwaili, Barcelona na Arsenal na mechi nyingine ni Juventus na Bayern Munich.
Magoli ya Barcelona yalifungwa na wachezaji Neymar da Silva Santos, Luis Suarez na Lionel Messi akahitimisha idadi ya mabao hayo dakika ya 88.

Na goli pekee la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Mohamed Elneny dakika ya 51 kipindi cha pili.

Barcelona imeifunga Arsenal jumla ya mabao 5-1 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa dimba la Emirates.Katika mchezo mwingine Bayern Munich imepata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Juventus ya Italia.

Mabao ya Bayern yamefungwa na Lewandowski, Thomas Muller, Thiago Alcantara na Kingsley Coman, huku magoli ya Juventus ya kifungwa na Paul Pogba, na Juan Cuadrado.

Kwa matokeo hayo Bayern imeshinda jumla ya bao 6-4 kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.