Man U Wajipanga Kuivaa Livepool Leo, Jionee Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man U Wajipanga Kuivaa Livepool Leo, Jionee Hapa

Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za Uefa Europa Ligi zinatarajia kuendelea leo March 17 kwa mechi mbali mbali mechi ambayo wengi wana subiria kuona kama United itaweza kuifunga Liverpool ili kusongo mbele.
Manchester United na Tottenham zote ziko Viwanja vya Nyumbani kwao vikidaiwa kushinda kwa ushindi wa kishindo ili kutinga Robo Fainali kufuatia vipigo katika Mechi zao za kwanza.
Tottenham, maarufu kama Spurs wako kwao White Hart Lane Jijini London kurudiana na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund ambao walishinda Mechi ya kwanza 3-0 na hivyo Spurs wanapaswa kushinda 4-0 ili kusonga.
Nako huko Old Trafford ni marudiano ya Mahasimu wakubwa wa Soka la England ambapo Man United wanatakiwa waifunge Liverpool 3-0 ili wasonge baada ya kutandikwa 2-0 Wiki iliyopita huko Anfield kwa Bao za Penati ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.