Mambo ni Magumu Kwa Chelsea - Hiddink - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mambo ni Magumu Kwa Chelsea - Hiddink

Kocha wa muda wa timu ya Chelsea, Guus Hiddink amekiri kuwa ni ngumu kwa timu yake kuingia kwenye nne bora ya ligi nchini Uingereza msimu huu.
Baada ya kutoka Chelsea kutoka sare kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge kwa kufungana goli moja kwa moja na timu ya Stock City, Guus Hiddink amesema ni ngumu kwa Chelsea kuingia kwenye nne bora msimu huu ambayo itaiwezesha timu hiyo kucheza michuano ya ligi ya mabingwa ulaya (Uefa) msimu ujayo.

“Nne bora haiwezekani tena, tulinusurika kuingia kwenye hatari ya kushuka daraja mwezi Desemba, na tumejiweka salama ndani ya muda mfupi sana,” alisema Hiddink.

“Kupanda katikati ya msimamo wa ligi, kwa kiwango cha kawaida cha Chelsea, haitoshi,” aliongeza.
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.