Lulu Atengwa Bongo Muvi, Wadai Habadiliki, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Atengwa Bongo Muvi, Wadai Habadiliki, Ipo Hapa

Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ameendelea kuzua minong’ono kutokana na kitendo cha kutoshiriki kwenye mikusanyiko ya wasanii wenzake hadi kufikia hatua ya kutengwa.

Hali hiyo ya sintofahamu ilijidhirisha Jumanne iliyopita kwenye hafla ya kumpongeza Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na wasanii wa Bongo Muvi chini ya uratibu wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ katika Hoteli ya Rodizio iliyopo Masaki, jijini Dar.

“Jamani! Mbona Lulu hajifunzi kutokana na makosa ? Juzi alipokuwa akirudi na tuzo kutoka Nigeria, hatukwenda kumpokea kutokana na yeye kutokupenda kujumuika na wasanii wenzake, angalia sasa, hata leo hajaja kama kawaida yake.

“Nilidhani atabadilika kumbe wapi. Anapaswa kubadilika sababu sioni cha kumzuia, mbona akialikwa kwenye pati za rafiki zake huwa anakwenda lakini sehemu kama hizi haji? Kilichotokea Airport ni funzo tosha, Mungu alimpa na akiendelea hivi siku atakumbana na majanga mazito atakosa wa kumsaidia,” alisikika mmoja wa wasanii waliokuwepo katika hafla hiyo.

Mara baada ya kupokea malalamiko hayo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka hivi:
“Sababu zangu kutohudhuria katika hafla zao wao wenyewe wanazijua na wakizijua wao inatosha siyo lazima nikwambie na wewe (mwandishi). Elewa tu hivyo.”

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.