Louis Van Gaal Amwagia Sifa Marcus Rashford, Adai Ni Mshambuliaji Mahiri - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Louis Van Gaal Amwagia Sifa Marcus Rashford, Adai Ni Mshambuliaji Mahiri

Kocha Louis van Gaal amekiri kuwa kinda wa Machester United Marcus Rashford ana kila kitu anachostahili kuwa nacho mshambuliaji mahiri.
Louis van Gaal ameyasema hayo baada ya mechi na mahasimu wao City baada ya kinda huyo kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi wa 1-0.
Bao la dakika ya 16 la Rashford lilitosha kuipa ushindi United na kupunguza pengo la pointi kwenye Premier League kati yake na City ambapo sasa Manchester United imeachwa kwa pointi moja tu.

Van Gaal akakiri kuwa chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 alijihakikishia namba mara tu alipomchezesha mchezo wake wa kwanza mwezi uliopita. Hadi sasa Rashford amesha funga mabao matano katika michezo nane aliyocheza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.