KR Mullah Adai Akinyoa Ndevu Zake, Anakufa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

KR Mullah Adai Akinyoa Ndevu Zake, Anakufa

Baada ya mashakibiki kupitia mitandao ya kijamii kumtaka msanii mpya ya Radar Entertainment KR Mullah kubadili muonekano wake pamoja na kunyoa ndevu, msanii huyo ametoa msimamo wake kuhusu muonekano wake.
Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumanne hii, KR amesema hawezi kubadili muonekano wake kwani hiyo ndio utofauti wake na wasanii wengine.

“Siwezi kubadili muonekano wangu hata hizi ndevu sitoi, hata unipe milioni ngapi sitoi ndevu,” alisema KR “ Ndevu zangu zinathamani kubwa sana, yaani ndio uhai wangu ukininyoa tu nakufa,” aliongeza KR.

Pia KR amedai ameteuliwa na CEO wa Radar Entertainment ‘TID’ kuwa rais mpya wa label hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.