Katibu Mkuu Chadema: Nilibuni Kauli Mbiu ‘Mabadiliko Lowassa’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Katibu Mkuu Chadema: Nilibuni Kauli Mbiu ‘Mabadiliko Lowassa’

Wakati wengi wakizidi kuhoji uwezo wa Katibu Mkuu mpya wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, kutokana na kutokuwa na jina kubwa katika uwanja wa siasa, mbali na elimu aliyonayo, kipaji chake na uwezo binafsi, vimezidi kufichuka.

Mwishoni mwa wiki, Chadema ilimteua Dk. Mashinji kuwa Katibu Mkuu mpya kushika nafasi ya Dk. Wilbroad Slaa aliyejiuzulu nafasi hiyo Julai 30, mwaka jana kwa kile akichodai kuwa ni utaratibu kutofuatwa wa kumkaribisha Edward Lowassa, aliyehamia katika chama hicho kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kisha kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Hata hivyo, wakati wengi wakihoji uwezo wake, imefahamika kuwa Dk. Mashinji kwa kushirikiana na kamati yake, ndiyo waliobuni kaulimbiu (slogan), ya `Lowassa Mabadiliko, Mabadiliko Lowassa,’ ambayo ilitumika katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana na kuwa kivutio kikubwa.

Akihutubia mamia ya wananchi wa Jiji la Mwanza katika viwanja vya Furahisha, Katibu Mkuu huyo, alisema: “Katika mkakati wetu kama kamati ya wataalam, tulileta kauli ya Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko, wameiiga, lakini hawawezi kuwa kama sisi, tunamaanisha mabadiliko tunayoyazungumzia na tutayatekeleza kimkakati na kimfumo zaidi.”

Mbali na hilo, kati hiyo ya ndiyo iliyofanikisha maafikiano tisa ya Ukawa pamoja na suala zima la chama kipi kipewe nafasi ya kusimamisha umeya katika umoja huo.

Kauli hiyo ambayo hadi sasa inatumika kwenye vikao vya ndani, nje na mikutano ya hadhara vya Chadema, alishirikiana na Kamati ya Wataalam ya Ukawa ambayo imekuwa ikibuni na kushauri mambo mbalimbali ya uendeshaji wa umoja huo.

Katika umoja huo unaohusisha vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD, kamati ya wataalam iliongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu na Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania, Dk. Rodrick Kabangila na Makamu akiwa Dk. Mashinji na Katibu alitoka CUF.

Chanzo: NIPASHE

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.