Juma Nature: Sina Mpango Wa Kumtafuta Fella, Labda Akinitafuta yeye Kibiashara. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Juma Nature: Sina Mpango Wa Kumtafuta Fella, Labda Akinitafuta yeye Kibiashara.

Bet Sasa
Msanii wa muziki Juma Nature, amesema hawezi kumfuata bosi wake wa zamani Said Fella kumtaka afanye naye kazi tena kama zamani.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz Cha East Africa Television Alhamisi hii, Nature alisema kama akifuatwa na Fella kibiashara anaweza fanya naye kazi.

“Mimi siwezi kwenda kumuomba Fella nifanye naye kazi ila kama yeye ananitaka kibiashara aje tukae chini tuandikishane mkataba unaoeleweka hapo sawa lakini hivi hivi sina mpango wa kwenda kwake, maana najiamini na mambo yanakwenda vizuri,” alisema Juma Nature.

Katika hatua nyingine Juma Nature amesema kwa sasa amesharekodi kazi mpya na Shetta huku akidai video yake itakuwa habari ya mjini kwa namna ambavyo ameipangilia na mashairi yaliyo ndani yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.