JPM anasa kigogo TRA anayelipwa mishahara 17 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

JPM anasa kigogo TRA anayelipwa mishahara 17

Rais John Magufuli akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Chato mkoani Geita siku ya Jumanne

Rais Dk. John Magufuli, ameanika madudu aliyoyakuta ndani ya Serikali ikiwemo mmoja wa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kulipwa mishahara ya watu 17 na kuagiza mfanyakazi huyo afikishwe mahakamani.

Pamoja na hali hiyo amesema wapo watumishi wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi Sh milioni 40 kwa mwezi ambayo sasa itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi Sh milioni 15.

Rais Magufuli alitoa taarifa hiyo jana nyumbani kwake katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita ambapo alihutubia kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais.

Dk. Magufuli alisema Serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo.

“Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800 na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia Serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za Watanzania.

“Leo (jana) hii yupo mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato TRA ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17 na huyo ni lazima afikishwe mahakamani.”

“Serikali imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15,” alisema Rais Magufuli.

Alisema anashangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuishi kama malaika huku wengine wakiishi kama masheteni, jambo ambalo halina nafasi katika Serikali yake.

“Nyiye mliokuwa mnaishi kama malaika, sasa zamu yenu kuishi kama mashetani,” alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

Chanzo: Mtanzania

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.