Idris Sultan Adai Saa yake iitwayo "Richard Mille" Anayovaa Sio 'Feki' na inauzwa zaidi ya Tsh Bilioni 1. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Idris Sultan Adai Saa yake iitwayo "Richard Mille" Anayovaa Sio 'Feki' na inauzwa zaidi ya Tsh Bilioni 1.

“Big Brother Africa winner @idrissultan with the worst fake Richard Mille skull I’ve ever seen Skull has meth teeth and ate too much. That Hublot is missing some gold paint on the lugs as well,” waliandika.
Idris hakuwajibu moja kwa moja zaidi ya kuamua kuweka picha nyingine Instagram ikionesha saa zake hizo na kuandika:

It’s a new yet beautiful day. Count your blessings au fanya kama wasio kuwa na kazi hufanya “COUNTING OTHER PEOPLE’S BLESSINGS” soon soon soon kitaeleweka inshaallah, by the way wazungu wengi kwa page yangu leo njooni watanzania tutumie hii nafasi kuchukua maskolaship.”

Hata hivyo ujumbe huo wa Idris haukuweza kujibu swali la msingi, ni kweli saa zake ni feki?

“It’s real,” Idris ameiambia Bongo5 na kudai kuwa hakuinunua kwa fedha yake ya mfukoni hivyo hawezi kujisifia kuwa anaweza kuimudu.

Saa anayoizungumzia ni Richard Mille. Hii ni saa aghali na si rahisi mtu wa kawaida kuweza kuimiliki.

“Ni Richard Mille, RM052, it’s 518,000 dollars yaani kama one billion na ushee,” amesema.

Actually kwa msimamo wa madafu dhidi ya dola leo hii, saa ina thamani ya shilingi 1,276,000,000!

Idris ameipata wapi saa hii?

“Hakuna mtu wa kawaida anaweza kuamini kitu kama hicho,” anasema.

“Hata kwenye interview ya Nirvana wakati nafanya nilisema a president, tena nilikosea nilitakuwa kusema a kingndio alinipa kwasababu tulikuwa na a business deal tuliyokuwa tunashughulikia halafu kuna huyu mtu akaja wakati tumekaa pale mezani kwenye restaurant fulani tunaongea. Akaja akasema kuna saa hii hapa kuna mtu anaiuza, how much? Mimi sijui walikubaliana nini lakini mimi niliipenda, the king akasema unaipenda basi ichukue, mimi nikaichukua kwahiyo sijui hata aliinunua shilingi ngapi. Lakini nimekuja kugundua baadaye kuwa saa hii inauzwa kwa 518,000.”

Kwa upande wa ‘Fake Watch Busta’, Idris amesema hawezi kuhangaika kuwajibu kwakuwa anaamini unapokuwa na kitu halisi huhujitaji kusumbuka kuwathibitishia.

-bongo5
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.