Hivi Ndivyo Diamond Alivyomsaidia Chid Benz, Alimtoa Damu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hivi Ndivyo Diamond Alivyomsaidia Chid Benz, Alimtoa Damu.

Bet Sasa
Meneja wa wanamuziki wa bongo fleva Babu Tale ameweka wazi kitu ambacho watu wengi walikuwa hawakijui kuhusu Diamond na Chid Benz.

Akiongea kwenye kipindi cha eNews kinachorushwa na East Africa Television, Babu Tale ameweka wazi kuwa Diamond Platnums ambaye anamsimamia, alishawahi kumsaidia Chidi Benzi kuacha madawa, kwa kwenda kumtoa damu na kumuwekea damu safi, lakini jambo hilo lilikuwa la siri ndio maana aliweza kurudia.

“Diamond alimshamtoa Chidi damu, kutoa ile yenye madawa, lakini alirudia unajua Chid anaacha na kurudia, sasa labda ndio maana ilikuwa rahisi kwa yeye kurudi kwa sababu ilikuwa siri, Damond siku hiyo alishinda hospitali kutwa nzima, akimtoa Chidi damu”, alisema babu tale.

Kwa sasa Chid Benzi amepelekwa Rehab bagamoyo baada ya kurudia matumizi ya madawa ya kulevya, na kumuathiri kwa kiasi kikubwa, na ameahidi kuacha matumizi ya madawa hayo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.