Hii Hapa Orodha ya Matajiri Duniani, Bill Gates Aendelea Kuwa Juu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hii Hapa Orodha ya Matajiri Duniani, Bill Gates Aendelea Kuwa Juu.

Mtandao wa Forbes hivi karibuni umetoa orodha mpya ya watu matajiri zaidi duniani huku tajiri Bill Gates kutoka nchini Marekani anaendelea kuwa mtu tajiri zaidi duniani kwa utajiri wa dola bilioni 75, licha ya kupungukiwa dola bilioni 4.2 kutoka mwaka jana.

Ameendelea kuwa namba moja kwa miaka mitatu mfululizo. Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg amekuwa na mwaka bora zaidi kuliko mabilionea wote.

Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 31, ameongeza dola milioni 11.2 kwenye utajiri wake hadi kushika nafasi ya 6 kutoka nafasi ya 16 mwaka jana.

Hii hapa orodha ya watu kumi wa juu zaidi:

1. Bill Gates – $75bn – Marekani
2. Amancio Ortega – $67bn – Hispania
3. Warren Buffett – $60.8bn – Marekani
4. Carlos Slim Helu – $50bn – Mexico
5. Jeff Bezos – $45.2bn – Marekani
6. Mark Zuckerberg – $44.6bn – Marekani
7. Larry Ellison – $43.6bn – Marekani
8. Michael Bloomberg – $40bn – Marekani
9. Charles Koch – $39.6bn – Marekani
10. David Koch – $39.6bn – Marekani

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.