Good News: App ya Instagram Yaongeza urefu wa kupost video kutoka sekunde 15 hadi 60 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Good News: App ya Instagram Yaongeza urefu wa kupost video kutoka sekunde 15 hadi 60

Sasa unaweza kujiachia na kujinafasi. Watumiaji wa Instagram sasa wanaweza kupost video zenye urefu wa sekunde 60 kutoka sekunde 15 za awali.

Mabadiliko hayo yamefanyika kuanzia Jumanne hii kwenye app hiyo ya iOS na Android na yataanza kupatikana kwa watumiaji wote duniani miezi ijayo.

Miezi miwili iliyopita, Instagram iliwezesha matangazo kuwa na urefu wa dakika moja lakini sasa hata watumiaji wwa kawaida wataweza kufurahia mabadiliko hayo.

“We want to bring you fun, flexible and creative ways to create and watch video on Instagram,” kampuni hiyo imesema kwenye post yake. “Longer videos mean more diverse stories from the accounts you love, whether it’s Selena Gomez hanging out with friends or beauty star Bretman Rock’s latest makeup tutorial.”

Video zimekuwa muhimu kwenye app hiyo yenye watumiaji milioni 400 duniani. Uwezo wa kuweka video ndefu, kutawafanya watumiaji kutumia muda mrefu kwenye app.

Tayari Diamond aliyepo ziarani Ulaya ni miongoni mwa watu walioanza kufaidi huduma hiyo.

“From 15 seconds to 1minute!!!..Mwe! Asante Insta kwa kutuongezea urefu wa hizi clip tujinafasi,” ameandika kwenye video aliyoiweka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.