EWURA Yapunguza Bei ya Mafuta. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

EWURA Yapunguza Bei ya Mafuta.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema kuanzia tarehe 2 Machi bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 2016.

Kwa Machi 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’

“Kwa kiasi kikubwa, kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia,” alisema Ngamlagosi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.