Diamond: Sikutegemea ‘Zigo Remix’ ingekiki hivi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond: Sikutegemea ‘Zigo Remix’ ingekiki hivi

Zigo Remix ni moja kati ya nyimbo ambazo AY hapaswi kuzisahau.

Mpaka sasa video ya wimbo huo inakaribia miezi miwili tangu itoke. Kwenye mtandao wa Youtube imeshafanikiwa kutazamwa kwa zaidi ya mara milioni nne.

Akiongea kwenye collabo ya Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema ‘sikutegemea kama wimbo wa Zigo Remix ungekuwa hivi kwa sababu jinsi tulivyorekodi inafurahisha.”

“AY hakuniambia moja kwa moja kama kuna wimbo tunatakiwa kufanya, aliongea na menejimenti yangu kwanza japo mimi na yeye tuna mawasiliano ya karibu,” ameongeza.

“Wakati naelekea Afrika Kusini kushoot video ya Mafikizolo na Utanipenda, niliandika baadhi ya mistari ya kwenye ‘Zigo Remix’. Tulivyofika Afrika Kusini AY alinunua baadhi ya vifaa vya studio, tukakaa dinning na kuanza kuingiza vocal kesho yake tukaenda kushoot video. Tulivyofika bongo tukaingiza vocal upya kwa sababu tulivyoingiza kule haikuwa nzuri sana.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.