Babu Tale: Kama Wewe ni Msichana na Unamzidi Ruby Kuimba Njoo WASAFI Records - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Babu Tale: Kama Wewe ni Msichana na Unamzidi Ruby Kuimba Njoo WASAFI Records

Meneja wa lebel ya WCB Babu Tale ametoa fursa kwa wasanii wa kike wenye vipaji kuonyesha vipaji vyao, na hatimaye kuweza kupata fursa ya kuwa chini ya uongozi wao wa WCB.

Babu Tale ametoa fursa hiyo alipokuwa akiongea ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio, alipoenda kumtambulisha msanii mpya amabye atakuwa chini ya uongozi huo Raymond TipTop, na kusema kuwa wasani wa kike ni wachche hivyo wana fursa kubwa ya kufanya vizuri iwapo watajituma.

Tuna Plan kuwapata wasanii wa kike lakini wenye vipaji vya ukweli, asikwambie mtu industry yetu ina wanawake wachache, tungepata wananwake wanne hata watano', alisema Babu Tale
Pia babu Tale alisema anatamani sana msanii Ruby angekuwa kwenye management yake, kwani ana uwezo mkubwa lakini kwa bahati mbaya ytayari yuko chini ya management nyingine ya THT.
Kwangu mimi ingekuwa Ruby hayuko chini ya THT, au hana management tungemchukua, lakini nasema hivi, kama anakuja mwanamke, awe na level ya kufanana na Ruby au kumshinda Ruby", alisema Babu Tale

Pamoja na hayo nae Diamond Platnums amesema ameweka wazi vigezo ambavyo msanii huyo wa kike avifikie ili aweze kuwa chini ya uongozi huo, pamoja na kujituma tofauti na walivyozoea kuwa hawawezi.

Aweze kuandika mashairi, aandike nyimbo zake mwenyewe unajua kuna kitu kimoja, wanawake washajiwekea kuwa wao hawawezi, sio kweli hawataki kufocus na kujaribu", alisema Diamond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.