Baada ya Wimbo Lupela, Alikiba Anakuja Tena Kivingine. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Wimbo Lupela, Alikiba Anakuja Tena Kivingine.

Mwanamuziki Ali Kiba ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya Lupela amefunguka na kusema kazi nyingi zinakuja ila kwa sasa atatoa kazi na wasanii kutoka nchini Kenya wanaounda kundi la Sauti Sol.
Akipiga stori kupita kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV Ali Kiba amesema baada ya kazi yake hii inayotamba sasa wataachia kazi ya kushirikiana ambayo imefanywa na nchini Kenya na ameshirikiana na kundi la Sauti Sol. AliKiba alidai wimbo huo tayari umekwisha kamilika na tayari wameshafanya mpaka video ya wimbo huo hivyo wanasubiri wakati tu.

“Kazi zipo nyingi zinakuja ila baada ya Lupela tutaachia kazi ya pamoja kati yangu mimi na kundi la Sauti Sol ambayo imeshakamilika na video tayari tulishafanya hivyo muda ukifika tutawajuza mashabiki wetu” Alisema Ali Kiba.

Ali Kiba ni miongoni mwa wasanii ambao wamefanya vizuri kwa mwaka jana kwenye muziki na bado anaendelea kufanya vyema kwa mwaka huu, kwa kazi yake na Christian Bella pamoja na Lupela.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.