Alikiba Kupiga Show Tuzo za AMVCA 2016, Lagos Nigeria Kesho 5 March. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba Kupiga Show Tuzo za AMVCA 2016, Lagos Nigeria Kesho 5 March.

Alikiba akiwa kwenye mazoezi kujiandaa na show.
Alikiba ni mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards, AMVCA 2016 zinazotarajiwa kutolewa Jumamosi hii jijini Lagos, Nigeria.

Tuzo hizo kubwa za filamu Afrika, zitaoneshwa live kupitia channel ya Africa Magic na Maisha Magic East kwenye DSTV.

Kwenye tuzo hizo, waigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Single ‘Richie’ Mtambalike na Yvonne ‘Monalisa’ Cherry walitahwa kuwania.

Lulu alitajwa kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha Best Movie – East Africa kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu pamoja na Monalisa kupitia Daddy’s Wedding.

Naye Richie alitajwa kupitia filamu ya Kitendawili ambapo pia ilitajwa kuwania kipengele cha ‘Best Indigenous Language Movie/TV Series.’


-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.