'Wakati mwingine unaweza ukajiona umempata kumbe umepatikana' - Wolper - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

'Wakati mwingine unaweza ukajiona umempata kumbe umepatikana' - Wolper

Staa wa filamu Jacqueline Wolper ameibua maswali mengi kwa mashabiki wake wa filamu katika mitandao ya kijamii baada ya kuandika ujumbe unao onyesha huenda ametendwa katika mapenzi.
Muigizaji huyo ambaye mwisho wa mwaka jana (2015) alimtambulisha mpenzi wake mpya kwa mashabiki wake baada ya kuvalishwa pete, Ijumaa hii ameweka wazi yale yanayomsibu moyoni hali iliyowafanya mashabiki wake watafsiri ametendwa.
Kupidia instagram, Wolper ameandika:

"Maisha yana mitihani migumu saana wakati mwingine unaweza kujiona umempata kumbe umepatikana. Unaweza hata kukufuru Mungu lakini kuna kale kausemi kanachosema tunajifunza kutokana namakosa me nimeanza kuzingatia misemo baada yakukua mkubwa.
Unaweza ukahsi unaishi na mjusi kumbe unaishi na nyoka mwenye sumu kali akikung’ata auponi ewwwe Mungu nipe nguvu eewe Mungu wangu nitoe upofu eewe Mungu washa taa kwenye giza nene nililopo ili nipate muangaza."

Mbali na staa huyo kutofanya mawasiliano na muandishi wa habari yeyeto kuhusiana na post hiyo pia ameandika...

"Some people are just waiting for that sad news about you. May they wait till they perish #mtu akifunguka kidogo mnajiongeza namnayoyajua dah kweli waTz insta mzungu alituletea sisi natujipigie makofi kwa hili..."

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.