Vanessa Mdee amjibu shabiki aliyemtaka atoe sadaka. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vanessa Mdee amjibu shabiki aliyemtaka atoe sadaka.

Msanii wa mziki wa bongo fleva Vanessa Mdee, anayefanya vizuri na wimbo wa “Never Ever” ametoa jibu ambalo limeonekana kuwavutia wengi kwenye mtandao wa twitter baada ya moja ya mashabiki kum tweet kwamba awe anasaidia maskini badala ya kuonesha ufahari kwenye mtandao.

Tukio hilo lilikuja baada ya msanii huyo kupost vocha kadhaa na kuandika ..”Jamani na hizi za Voda kwa anayehitaji vocha   #MoneyMondays “ndipo shabiki mmoja akamjibu.. “Its better ukatoa sadaka kwa maskini wasojiweza kuliko kuonyesha ufahari kwenye social media Vanessa, hizo vocha hazisaidii.”

Jibu la Vanessa lilisomeka kama ifuatavyo.. “Sadaka zenye baraka ni zile zinazotolewa bila kutangazwa wewe tengeneza maisha yako and i’ll do the same,” kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.