Tuddy Thomas Afunguka Kuhusu Kushindwa Kupiga Kinandani Vizuri, Amshukuru Diamond Kwa Kumwamini. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tuddy Thomas Afunguka Kuhusu Kushindwa Kupiga Kinandani Vizuri, Amshukuru Diamond Kwa Kumwamini.

Prodyuza Tuddy Thomas toka studio za Epic rekodi amefunguka na kusema kwa sasa anapata wakati mgumu sana kupiga kinanda,hiyo inatoka na maumivu aliyo nayo baada ya kuvamiwa na majambazi katikati ya mwaka jana na kupata majeraha kadhaa.

“Hakuna kitu kinaniuma kama upigaji wa kinanda vizuri, nimekuwa sina uwezo wa kupiga kinanda vizuri nakuwa nadokoa sana,kama nyimbo nilikuwa napiga kwa dakika tano sasa hivi nafanya kwa lisaa na nusu…Sometime huwa nikikaa kufikiria nalia sana” amefunguka Tuddy.


Hata hivyo Tuddy amemshukuru msanii Diamond kwa kumtia moyo na kumwamini na kumfanya aweza kupiga kinanda vizuri kwenye wimbo wa Je Utanipenda.”Wakati nafanya kazi na Diamond,Je Utanipenda nilimwita Emma aje apige kinanda ila Diamond akanambia,unajua Tuddy unatachi za peke yako,akataka nipige vile vile japo ilikuwa kidogo na kwa ugumu“aliongeza Prodyuza huyo na kuwashukuru wasanii wanaoendelea kumwamini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.