Shilole, Nuh Sasa Kuringishiana Wapenzi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole, Nuh Sasa Kuringishiana Wapenzi.

Baada ya hivi karibuni Shilole na Nuh Mziwanda kumwagana kisha kila mmoja kumwanika mpenzi wake mpya, sasa wasanii hao imekuwa ni full kuringishiana huku kila mmoja akidai amepata mtu sahihi

Shilole akiwa na mpenzi wake mpya.

Nuh juzikati alisema kuwa, kwa Shilole alikuwa kapotea njia na sasa amempata mwenza sahihi aitwaye Erah Erah huku Shilole naye akitamba kuwa, mwanaume aliyempata ambaye anafahamika kwa jina la Medy Music ana kila sifa ya kuwa mume tofauti na Nuh.

“Hapa nimefika, huyu sasa ndiye mume wangu,” alisema Shilole kwa kifupi.

Hata hivyo, rafiki wa karibu wa Nuh aliitonya safu hii kuwa, kila wanapokutana wasanii hao wakiwa na wapenzi wao inakuwa ni mwendo wa kurushana roho tu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.