Shamsa Ford: Siwezi Kurudiana na Nay wa Mitego - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford: Siwezi Kurudiana na Nay wa Mitego

Bet Sasa
Ikiwa imepita siku moja toka Nay wa Mitego kupost picha ya Shamsha Ford kwenye mitandao yake ya kijamii ikiwa na ujumbe wa ‘Happy Valentine’ hususani siku ya wapendanao mwanadada Shamsha Ford amefunguka na kusema kuwa kamwe hawezi kurudiana kimapenzi na msanii huyo wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Shika Adabu yako’,

Shamsha Ford amesema kuwa kwa sasa ana maisha yake na mwanaume mwingine ambaye wanaheshimiana na anampenda hivyo kitendo cha Nay kupost ujumbe wa Valentine akitumia picha yake yeye anaona ni kama msanii huyo anataka kuwakumbusha watu mambo ambayo yeye alishayasahau na mashabiki walisha sahau na kumtaka msanii huyo amuheshimu kwani kwa sasa hayupo kutafuta kiki wala scandal za kijinga.

“Naona mambo yanazidi kuvumishwa kwamba nimerudiana na Nay. Pls pls nina maisha yangu na mwanaume ambae nampenda na kumuheshimu. ..sijarudiana na nay na haiwezi kutokea kabisaaa. ..Nay una ndugu na marafiki wengi wa kuwaposti siku ya leo haikuwa muhimu uniposti mimi. nilishukuru Mungu watu walishasahau kuhusu mimi na wewe but naona umetaka kuyafufua. Sipendi scandal na si maisha yangu kutafuta kiki za kijinga. KAZI YANGU NDO INAYONITAMBULISHA. ..PLS TUESHIMIANE” alimalizia Shamsa Ford.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.