Rihanna na Drake na wamerudiana na kuwa wapenzi tena ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rihanna na Drake na wamerudiana na kuwa wapenzi tena ?


Huenda Rihanna na Drake hawajaishia kushirikiana kwenye wimbo mpya tu, Work, bali wakawa wamerudiana tena, kwa mujibu gazeti la The Sun.
Chanzo kimoja kililiambia gazeti hilo kuwa wamerudiana. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, siku mbili kabla ya kutumbuiza pamoja kwenye Brit Awards Jumatano, wawili hao walijirusha pamoja kwenye klabu ya usiku jijini London.

The Sun pia iliongeza kuwa wawili hao hawakuonesha mapenzi yao na walipigana busu wakati wakicheza. Rihanna, 28 na Drake, 29, walirudisha tetesi za kuwa na uhusiano baada ya wawili hao kushirikiana kwenye wimbo Work.

Hakuna yeyote kati yao aliyethibitisha kuwa wamerudiana.

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa ex wa Rihanna, Chris Brown alikasirika kutoka kwa single hiyo kwakuwa alihisi wawili hao walitoa kumkasirisha.
-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.