Rais Magufuli panda ndege nenda nje ukajifunze dunia inavyokwenda – Sugu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rais Magufuli panda ndege nenda nje ukajifunze dunia inavyokwenda – Sugu

Bet Sasa

Sugu anahisi ni muda sasa Rais Dkt John Pombe Magufuli akapanda ndege na kwenda nchi za nje kujifunza namna ambavyo nchi zingine zinaendesha uchumi wake na mambo mengine.
Mbunge huyo wa Mbeya Mjini ambaye jina lake ni Joseph Mbili amesema safari za nje sio tatizo na kwamba baadhi ya gharama haziepukiki.

“Ili twende sambamba na dunia, sisi sio kisiwa, ni lazima Rais Magufuli aende UN, lazima aende AU kwenye vikao vya kimataifa. Sasa hivi kuna mkutano Davos wa kimataifa, dunia yote ipo kule inazungumzia uchumi yeye amekaa huku,” alisema Sugu bungeni wiki hii.

“So president Magufuli has to go abroad, akajifunze, take a jet brother, he has to take a jet akajifunze dunia inafanya vipi, marais wengine wanafanya vipi,” aliongeza.

Sugu alidai kuwa safari za nje kwa rais ni muhimu ila anachotakiwa ni kupunguza tu watu watakaoongozana naye.

Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli hawajawahi kusafiri nje ya nchi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.