Picha 4 za mfano wa gari la kifahari Diamond Platnumz analotaka kulinunua mwaka huu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha 4 za mfano wa gari la kifahari Diamond Platnumz analotaka kulinunua mwaka huu.


 Mwimbaji kutoka kwenye muziki wa bongofleva Diamond Platnumz alikaa kwenye Exclusive Interview ya onAIRwithMillardAyo na kuzungumza vitu vingi sana kuhusu maisha yake na muziki wake ambapo moja ya maswali aliyoyajibu kwa kujiachia na akiwa ana tabasamu ni kuhusu kununua gari la ndoto yake.
Platnumz alimwambia Millard Ayo >>> ‘Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekua ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokua nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakua na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida’
‘Mbali na kuwa msanii nimeshakuwa C.E.O sasa na kuna baadhi ya vikao ukija na gari ya kitoto huwezi kufanya dili vizuri, kuna baadhi ya sehemu siwezi kwenda naendesha mimi… pia siwezi kuendeshwa nikiwa nimekaa kwenye X6naonekana kama muhuni tu… ndio maana nikipata Rolls royce inatengeneza heshima‘ – Diamond 
R2
Picha zote hizi ni mfano wa aina ya gari analotaka kulinunua Diamond Platnumz.
R1
-millardayo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.