Nuh Mziwanda " Shilole amekuwa adui yangu, anabana kila sehemu " - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nuh Mziwanda " Shilole amekuwa adui yangu, anabana kila sehemu "

Msanii wa muziki Nuh Mziwanda amedai kuvunjika kwa uhusiano wake na Shilole kumezaa uadui kati yao.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Jumatatu hii, Nuh alidai imefikia hatua Shilole amehack akaunti yake ya istagram.
“Baada ya mapenzi kuisha mi nimekuwa adui yake, amehack akaunti yangu ya instagram. Najaribu kuwacheki watu wa kuirudisha akaunti yangu wanashindwa kunirudishia anabana kila sehemu,” alisema
“Kuna vitu ananifanyia vidogo vidogo ambavyo nimefanya kugundua kuwa hakuwa mwanamke mzuri kwangu, alikuwa anashindwa kuonesha true colour yake nimekuja kuijua baada ya kuachana naye”, alisema Nuhu.
Katika hatua nyingine Nuh alisema iwapo wangeachana kwa amani na Shilole asingelazimika kuifuta tatoo ya mpenzi wake huyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba amemsaidia katika maisha yake.
“Mi ningeiacha tatoo kama Shishi ningeachana nae poa, kila mtu na maisha yake fresh tukionana tunasalimiana hakuna noma, lakini mwenzangu kwenye interviews anasema, akiitwa kwenye interview anaongea hiki kwamba mimi sina kitu, sijui nashindwa kusurvive nakula magengeni, anaongea vitu vingi ambavyo anajaribu kutoa fan base yangu, angekuwa mtu mzuri baada ya kuachana naye, tatoo ningeiacha kwa sababu ningejua bado kabaki kuwa rafiki yangu na ni mtu ambaye alinisaidia”, alisema Nuh.
Hata hivyo Nuh alisema yeye binafsi hana chuki na msanii huyo ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.