Niva Aanika Siri za Nay wa Mitego Ikiwemo Kupigwa Kibuti na Shamsa Ford. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Niva Aanika Siri za Nay wa Mitego Ikiwemo Kupigwa Kibuti na Shamsa Ford.

Baada ya Nay wa Mitego kumchana staa wa bongo muvi,Niva super mario kuwa ‘hana pa kulala,analala kwenye gari’ kupitia wimbo wake wa shika adabu yako,Niva amejitokeza na kurusha madongo kadhaa kwa msanii huyo anayejiita rais wa manzese.

Kupitia mahojiano yake na kipindi kimoja cha redio Niva ameweka wazi kuwa hajaanza kumfahamu leo Nay na yeye amekuwa akimjua kwa jina la ‘Imma Chogo‘ na amewahi kumsaidia mambo kadhaa ikiwemo kulala kwake na kushangaa anasemaje yeye (Niva) hana pa kulala.

“Nay amewahi kuja kwangu mwaka 2012 ameibiwa kila kitu kwenye gari yake nikamsaidia tuka chill kwangu apoze machungu,kama sina pa kukaa pale alikuja kwa nani?” alihoji Niva na kuongeza “Sio hilo tu wakati wa kampeni Nay alivamiwa kwake,Dar akawa anataka msaada wa pesa nikatoa milioni mbili na nusu,na ndicho kipindi ambacho Shamsa alimpa kibuti kwenye ziara za kampeni,Mwanza kwa sababu hajielewi.” alimaliza Niva.

-Times Fm
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.