Mwanamuziki Wa Marekeni Ne-Yo Kutumbuiza Mwanza, May 21 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwanamuziki Wa Marekeni Ne-Yo Kutumbuiza Mwanza, May 21

Bet Sasa
Muimbaji wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo, anatarajiwa kutumbuiza jijini Mwanza, May 21.
Atatumbuiza kwenye tamasha kubwa la kila mwaka la Jembeka linaloandaliwa na kituo cha redio cha Jembe FM cha jijini humo.

Hii itakuwa mara ya tatu muimbaji huyo kuja Afrika Mashariki. Ameshatembelea Kenya alikoenda kwenye Coke Studio Afrika mwaka jana na Uganda alikoenda kutumbuiza.

Kwenye tamasha hilo pia, Diamond ambaye mwaka jana alimshirikisha msanii huyo atakuwepo.

Ni hivi karibuni tu kituo hicho kinachofanya vizuri jijini Mwanza kiliwaleta wasanii wa Nigeria, Seyi Shay na Tekno kwenye tamasha la utangulizi la Muzika lililofanikiwa.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.