Mdee, Kubenea washikiliwa na Jeshi la Polisi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mdee, Kubenea washikiliwa na Jeshi la Polisi

Mwenyekiti wa BAWACHA na Mbunge wa Kawe Halima Mdee
Mwenyekiti wa BAWACHA na Mbunge wa Kawe Halima Mdee
Wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia vurugu kutokea katika Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika siku ya Jumamosi.
Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuchochea vurugu zilizosababisha kujeruhiwa kwa mmoja wa kiongozi wa juu wa serikali.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Said Kubenea
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Said Kubenea
Kamanda Mkuu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema wabunge hao wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi.

-taarifa

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.