Mafikizolo: Collabo yetu na Diamond ni ‘moto wa kuotea mbali’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mafikizolo: Collabo yetu na Diamond ni ‘moto wa kuotea mbali’


Kundi la muziki la nchini Afrika Kusini, Mafikizolo, limedai kuwa collabo yao na Diamond Platnumz ‘Colors of Africa’ ni moto wa kuotea mbali.
Member wa kundi hilo, Theo, amedai hadi sasa video yake haijatoka kwakuwa wamepanga kitu kikubwa zaidi kwaajili ya kuifanyia promotion.

Theo alikuwa akimjibu shabiki aitwaye Frankestain Pastory, aliyemuuliza Instagram sababu za kuchelewa kwa video hiyo.

“Tunafahamu kuwa mashabiki wetu wanasubiri lakini tuna mpango mkubwa wa kimasoko kwaajili ya uzinduzi wa video,” alisema Theo.

“Mafikizolo na Diamond ni wanamuziki wakubwa sana Afrika hivyo uzinduzi wa wimbo na video yake unatakiwa kupangwa vyema. Ninachoweza kukuahidi ni kuwa video na wimbo vimesimama. Hatutowasubirisha kwa muda mrefu sana. Tafadhali kaka yangu kuwa mvumilivu, subira yako haitopotea bure.”
-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.