Mabishano makali kati ya Mdee na Mwakyembe bungeni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mabishano makali kati ya Mdee na Mwakyembe bungeni

Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee (Chadema), jana waliingia kwenye mvutano mkali huku wakitunishiana misuli ya sheria kuhusu kashfa ya ununuzi wa mabehewa 274 yanayodaiwa kuwa mabovu. Ununuzi huo uliofanywa wakati Dk. Mwakyembe alipokuwa Waziri wa Uchukuzi.

Mdee aliibua tena suala la kashfa ya ununuzi wa mabehewa hayo 274 akisisitiza kuwa ni mabovu, wakati alipopata nafasi ya kuchangia katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2011/- 2015/16 ambapo aligusia ahadi ya serikali ya kukarabati reli ya kati ambayo alidai haijatekelezwa ipasavyo.

Dk. Mwakyembe alikanusha taarifa ya kuwepo kwa mabehewa mabovu kati ya mabehewa hayo 274 yaliyonunuliwa wakati akiwa Waziri wa Uchukuzi.

“Leo nikimwambia Halima aniletee mabehewa ambayo hayafanyi kazi atashindwa kunionesha,” alisema Mwakyembe

Sikiliza mwenyewe hapa;

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.