Maalim Seif amlipua JK - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Maalim Seif amlipua JK

Bet Sasa

Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa madai mapya mazito kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yalipinduliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha, baada ya kupata baraka za Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Maalim Seif Alitoa madai hayo alipokuwa akizungumzia azimio la Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililoamua kususia uchaguzi ukuu wa marudio alipokutana na viongozi wa wilaya wa chama hicho, Unguja jana.

“Kitendo cha kupindua maamuzi ya Wazanzibari waliyofanya kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25, Desemba, mwaka jana kilifanywa kwa baraka zote za aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho Kikwete,” alisema Maalim Seif katika mkutano huo uliyofanyika Kiembe Samaki, mkoa wa mjini Magharibi, Unguja.

Huku wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika utulivu mkubwa, Maalim Seif alisema: “Hakuna mtu mbaya kwa Zanzibar na Wazanzibari kama Jakaya Mrisho Kikwete.”

Alisema mpango wa kufutwa matokeo ya uchaguzi huo umewa sababisha nchi kuingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisiasa baada ya kupata baraka za Kikwete akiwa wakati huo Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama.

Maalim Seif alidai mpango huo ulisukwa baada ya kuona Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika mazingira magumu ya kushindwa uchaguzi huo.

Aidha, Maalim Seif alisema viongozi na wanasiasa wanaosema Rais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli, hana mamlaka ya kuingilia suala la Zanzibar ni wanafiki wanaokwepa utatuzi wa mgogoro kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

“Uchaguzi wa marudio sio halali na si ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi uliopo kwani uchaguzi halali ulifanyika Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Maalim Sef ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ana aliyekuwa mgombea urais wa CUF katika uchaguzo huo.

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Alisema hakuna njia ya kumaliza mgogoro wa uchaguzi Zanzibar zaidi ya ZEC kukamilisha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana na kumtakngaza mshindi wa uchaguzi huo.

KUVUNJIKA MAZUNGUMZO
Kuhusu kuvunjika kwa mazungumzo ya kusaka muafaka wa mkwamo wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, Maalim Seif alidai chanzo ni Mwenyekiti wa mazungumzo hayo, Rais Ali Mohamed Shein, kwa kile alichosema hakuwa na nia njema na alishindwa kuonyesha ukweli katika kumaliza mgogoro huo.

“Ni mtu anayeamini kutawala kwa mabavu na matumizi ya nguvu na asiyejali wala kuheshimu Katiba ya nchi,” alisema.

Maalim Seif aliwataka wanachama na wafuasi wa CUF kuendelea kutembea kifua mbele wakijua wao ndiyo washindi halali wa uchaguzi huo.

Alisema iwapo CCM ikilazimisha kufanyika uchaguzi wa marudio na kumtangaza Shein kuwa Rais itakuwa ni kujidaganya kwa sababu Wazanzibari wanamjua nani Rais wao halali waliomchagua na kumpa ridhaa ya kuwaogoza katika kipindi cha miaka mitano.

Alisema msimamo wa CUF upo palepale wa kutoingia katika uchaguzi wa marudio kwa kuamini kuwa uchaguzi ulikwisha kufanyika Zanzibar.

Alisema hata ripoti za waagalizi wa kimataifa na wa ndani wa uchaguzi huo walisema ulikuwa huru na wa haki kabla ya Mwenyekiti wa ZEC kufuta kibabe matokeo ya uchaguzi huo.

Tangu ZEC ilipotangaza kuwa uchaguzi wa marudio utafanyika Machi 20, mwaka huu, kumeibuka mjadala mkubwa, baadhi ya wananchi wakiunga mkoni na wengine wakipinga kurudiwa kwa uchaguzi huo.

-NIPASHE

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.