Jose Mourinho afanya mazungumzo na Man United - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jose Mourinho afanya mazungumzo na Man United

Manchester United imefanya mazungumzo na wawakilishi wa kocha wa zamani Chelsea Jose Mourinho, BBC imetambua.
Mreno, 53, ambaye alitupiwa virago na Blues mwezi Desemba, anaendelea kuwa na matumaini ya kumrithi Louis van Gaal Old Trafford.
Mourinho alifukuzwa kazi Chelsea mwezi Desemba 2015

Hakuna makubaliano yaliyofiki, na klabu haijatamka lolote, lakini makubaliano yameanza.

Mholanzi Van Gaal, 64, anatarajiwa kuondoka United mwishoni mwa msimu – mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.
Louis van Gaal wa Manchester United anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Hiyo itamuwekea njia wazi Mourinho, ambaye anajulikana kuwa atafurahia endapo ataichukua Old Trafford.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.