John Terry huu ndo msimu wangu wa mwisho kubaki Chelsea - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

John Terry huu ndo msimu wangu wa mwisho kubaki Chelsea

Nahodha wa Klabu ya Chelsea John Terry anatarajiwa kuihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu inayo shiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
YOUNG CHELSEA DEFENDER JOHN TERRY PICTURED AT HARLINGTON TRAINING GROUND.PIC DAVE SHOPLAND
Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwisho wa msimu na hajapewa mkataba mpya kuna taarifa kutoka kwa uongozi kuwa hatoongezewa mkataba mpya kuendelea kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridges.
30C37C8600000578-0-image-a-38_1454265994254
Beki huyo mwenye miaka 35, aliyejiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 14, ameshinda Ligi ya Premia mara nne, Kombe la FA mara tano na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara moja akiwa na The Blues.
“Ningependa sana kuendelea kukaa, lakini klabu inaelekea upande tofauti,” amesema.
Terry amechezea Chelsea mara 696.
“Walisema kwamba meneja mpya akija, mambo huenda yakabadilika,” Terry alisema baada ya klabu hiyo kuifunga MK Dons 5-1 katika raundi ya nne Kombe la FA.
“Kwa sasa sijapata mkataba. Nilitaka kujua sasa kama ilivyokuwa awali kila Januari na hili huchukua miezi kadha kukamilishwa. Hautakuwa mwisho nilioutarajia. Sitastaafu soka nikiwa Chelsea, imechukua siku kadha kukubali hili.”
Baadaye hata hivyo, msemaji wa klabu alisema huenda Terry akapewa mkataba mpya.
“John ameshauriwa kwamba ingawa kwa sasa hajapewa mkataba wowote, kwamba hali inaweza kubadilika miezi kadha ijayo,” msemaji wa klabu hiyo alisema baadaye Jumapili.
“Klabu hii inamheshimu sana John na kuthamini yote ambayo ametusaidia kutimiza kufikia sasa.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.