IMEVUJA: Hii Ndio Siri ya Mwizigaji Ray Kuwa " Mweupe " - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

IMEVUJA: Hii Ndio Siri ya Mwizigaji Ray Kuwa " Mweupe "

Bet Sasa
Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Ray Kigosi amesema kwamba yeye hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi .

Ray ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV na kusema kwamba hua anakwenda salon mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.

Naye Mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba Mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.

Katika kipengele cha ''Cheche'' ambacho majirani hupewa nafasi ya kumzungumzia msanii au mgeni wa siku kwenye show wamesema kwamba Ray apunguze kutumia vipodozi kwani anakuwa kama mchina.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.