Idris, kakuhakikishia nani mimba ya Wema ni yako ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Idris, kakuhakikishia nani mimba ya Wema ni yako ?

Bet Sasa
WAKATI Mwisho Mwampamba aliposhiriki kwa mara ya kwanza Shindano la Big Brother miaka ile ya mwanzo wa 2000, Wabongo wengi hawakuwahi kufikiri kama ni kitu ambacho kingeweza kuwasaidia vijana wetu, hata pale dau kubwa la mshindi lilipotangazwa. Wengi walitazama zaidi katika maadili, kwa sababu kulikuwa na mambo mengi ambayo kwa utamaduni wetu, hayakustahili kuoneshwa katika televisheni kama yalivyokuwa yakifanyika.
Lakini taratibu wakajikuta wanaliona shindano hilo kuwa la kawaida, lenye ‘kuburudisha’ hasa baada ya ushindi wa Richard mwaka ule wa 2007.

Leo hii, vijana wawili wa Kitanzania tayari wameweka kibindoni jumla ya dola 400,000 kutoka shindano hilo, kwani Richard alichukua dola laki moja alipotwaa ushindi na Idriss Sultan, aliyeibuka namba moja mwaka jana, kwa pesa ya madafu, ana kama milioni 500 hivi!

Sasa Idriss amekuwa kijana maarufu sana katika jamii yetu, akiwa ngazi moja ya mastaa wenzake wengine wa Bongo Fleva, Bongo Muvi na kada nyingine za ustaa, maana hapa kwetu, umaarufu ni jitihada zako tu katika kujipromoti!

Kama kijana, ninajivunia Idriss, kwa sababu ameongeza idadi ya masupastaa, lakini pia kiasi cha fedha alizopata zimechangia kuwagawia Watanzania wengine kwa namna moja au nyingine kwa vile nina uhakika, mshindi wetu huyu, ana kitu anakifanya na fedha zake, ambacho kwa vyovyote amewapa ajira wenzake, hata kama siyo ya kudumu.

Lakini nje ya ustaa, nina ushauri ninaopenda kumpatia na hasa kwa kuwa ninaamini bado ni bwana mdogo kiumri, hivyo kuna mambo ambayo hayahitaji fedha ili kuyapata, isipokuwa yanahitaji kujiongeza tu kiakili.

Yeye amethibitisha katika vyombo kadhaa vya habari kuwa hivi sasa anatoka na Wema Sepetu, ambaye naye ameutangazia umma kuwa ni mjamzito. Ni jambo la kheri kwake, hasa kwa vile kwa miaka mingi, wapinzani wake wametumia kukosa kwake mtoto kama fimbo ya kumchapia.

Ambacho hakijakaa sawa kwangu, ni kauli ya Idriss kuwa mimba ya Wema ni yake. Sibishi, lakini kuna vitu ambavyo mwanaume hatakiwi kupaza sauti, hasa unaposhiriki mapenzi na mwanamke wa aina ya Wema. Historia ya muigizaji huyu staa kimapenzi, inaonesha amekosa utulivu.

Ni kujilipua kwa kiwango cha juu, mtu kuja na kutoa kauli ya kujiamini kiasi hiki na tena mtu huyo anapokuwa kijana mdogo kama Idriss. Anayejua baba wa mtoto ni mama na kwa wasichana wa Kibongo, mtu kupewa ujauzito wala siyo suala la kuuliza.

Siku zote mwanaume anapaswa kuwa mtulivu kichwani, hasa anapozungumza mambo ambayo siku moja yanaweza kumgeuka. Sisemi kwamba amebambikwa, la hasha, ninachosema hapa ni umuhimu wa kuchukua tahadhari katika matamshi.

Na hii ni kwa sababu Wema ni rafiki yake tu, angekuwa amemuoa, yupo ndani kwake muda wote ingeweza kuwa sawa, lakini hawa dada zetu ambao wakati mwingine inapita hata wiki hujaonana naye, maneno haya ni ujasiri wa hali ya juu.

Hivi siku moja ikatokea wamekorofishana (na hili linawezekana kabisa) halafu huyu binti akaamua kumvua nguo na kumwambia mimba haikuwa yake, itakuwa aibu yake au yetu?
Maneno kama haya hutakiwi kutamka hadharani, unaiambia familia yako, jamani eeeh, ule mzigo wa Wema ni wanguu! Halafu walimwengu unawaacha wenyewe wajikanyage, wakisema ni wa kigogo wewe sawa, wakisema sijui ni ya nani wewe hewala, kwa sababu siku likisanuka, utakuwa salama mbele yao !
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.