Diamond Azungumzia Collabo na Yemi Alade na Jinsi Zari Alivyobadilisha Maisha Yake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Azungumzia Collabo na Yemi Alade na Jinsi Zari Alivyobadilisha Maisha Yake.

zari na diamond platnumz
Diamond Platnumz na msanii kutoka nchini Nigeria Yemi Alade wanatarajia kuja na collabo mpya.
Taarifa hiyo imetolewa na muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ alipokuwa akiongea na na D’Mike wa kipindi cha Mseto cha Radio Citizen. Amesema yeye na Yemi tangu wakutane kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, wameendelea kuwa washkaji wa karibu.

“Wiki mbili zilizopita amenitumia nyimbo yake mpya ambayo tutafanya, na ukiisikiliza hiyo nyimbo ina mahadhi ya kinyumbani East Africa kabisa, siwezi kusema jina inaitwaje japokuwa jina pia ni la Kiswahili,” alisema Diamond.

Katika hatua nyingine, Diamond alieleza jinsi ambavyo Zari amebadilisha maisha yake.

“Kwenye siku hii nzuri maalum ya Valentine’s kitu kikubwa nitakachoweza kumwambia [Zari] ni kwamba nampenda sana na kiukweli amecheza part kubwa sana katika maisha yangu mpaka hapa nilipo,” amesema.

“Amenizalia mtoto ambaye nilikuwa na ndoto hiyo siku zote na kila siku amekuwa akinifanya napevuka kwasababu nakuwa na akili za kimaisha natoka katika utoto nakuwa katika utu uzima ambao unanifanya niweze kutengeneza hata misingi mizuri ya kazi yangu pia. Ukisikiliza nyimbo zangu, strategy zangu za kimuziki zinazidi kupevuka. Ananitunzia moyo wangu vizuri sababu nina mapenzi naye mazito.”

Msikilize zaidi hapo chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.