D'Banj Amuhitaji Don Jazzy Afunguka Haya Stejini. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

D'Banj Amuhitaji Don Jazzy Afunguka Haya Stejini.

Bet Sasa

Mkali wa Muziki wa Pop nchini Nigeria DAPO OYEBANJO maarufu kama D'BANJ amefunguka kuwa yupo tayari kufanya ngoma na mkali BOSS wa MARVIN RECORDS DON JAZZY.

D'Banj alitamka maneno hayo akiwa moja ya walio-Perform juzi usiku kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa Seneta BEN MURRAY BRUCE, aliyewataka wakali hao kufanya japo Singo moja na D'banj alijibu kwa kusema, nimelifikiria sana hili kabla sijaja hapa jukwaani nilienda kwa Don Jazzy na kumuomba aungane na mimi hapa, nilimwambia kama akinipa Beat leo nyimbo itakuwa tayari siku inayofata,
"I have given serious consideration to this. Before I came on stage, I went to Don Jazzy and asked him to join me on stage. If he gives me a beat today, the song will be ready the next day. Alisema D'Banj

Si mara ya kwanza kwa wakali hao kutakiwa kurudiana kwa japo ngoma moja, ikumbukwe kwenye siku ya Kuzaliwa msanii 2FACE, 2face alitoa tamko la kuwataka wakali hao kufanya kazi angalau moja na D'Banj alionesha kulipokea fresh ila Don Jazzy hakuonesha kukubaliana na hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.