Ben Pol: Kuchora Tattoo, Kuvaa Hereni na Kufuga Rasta ni Mwiko Kwangu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ben Pol: Kuchora Tattoo, Kuvaa Hereni na Kufuga Rasta ni Mwiko Kwangu.

Msanii wa muziki wa R&B Benard Paul ‘Ben Paul’, amesema hapendi kuchora tattoo, kuvaa hereni pamoja na kusuka rasta kama baadhi ya wasanii wanavyofanya kwa kuwa ana uheshimu sana mwili wake.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.

“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alisema Ben Pol.

Ben Pol na Jux hivi karibuni wameachia wimbo wao mpya uitwao ‘Nakuchana’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.