Batuli kumpeleka Ray Kigosi kwenye vyombo vya sheria. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Batuli kumpeleka Ray Kigosi kwenye vyombo vya sheria.

Msanii wa filamu, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema ni muda mrefu amekuwa akivumilia maneno ya dharaua liyokuwa akijibiwa wakati akihitaji malipo yake kwa msanii mwenzie Vicent ‘Ray’ Kigosi.
Akizungumza kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm, Batuli amedai kuwa pesa anayomdai Ray ni milioni 1 na laki 2, malipo halali kwa vipande alivyoshiriki kwenye filamu ya Ray.

“Nikimpigia anaesema ana pesa, namwambia ungekuwa unahela usingeniita kwenye kazi yako.” alisema Batuli
Aliongeza, “Mi nikapata accident ya moto, nikamwambia naomba pesa yangu, akasema njoo upige picha ya ‘Cover’ nikasema sipigi mpaka unipe pesa yangu akanijibu ‘unaumwa wewe’, uvumilivu umefika kikomo nimeamua nitafute msaada wa kisheria na mkataba wangu umeungua kwenye ajali ya moto.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.