Bangi za Chris Brown zamsababishia pumu Royalty – Nia Guzman - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bangi za Chris Brown zamsababishia pumu Royalty – Nia Guzman

Mrembo aliyezaa na mwanamuziki Chris Brown, Nia Guzman amemtupia lawama mzazi mwenzake huyo kwa kumsababishia binti yao ugonjwa wa Pumu.

Nia Guzman amemlalamikia Brown kuwa amemsbabishia ugonjwa wa Pumu Royalty mwenye umri wa mwaka mmoja kutokana na moshi wa bangi na sigara anavyovuta.
Chris Brown akiwa na binti yake Royalty.

Nia anasema kila Royalty anaporejea kutoka kwa Chris mara nyingi anakuwa ananuka moshi na katika madai yake ya kisheria amesema ana wasiwasi mzazi mwenzake huenda anatumia madawa ya kulevya na anataka asiruhusiwe kukutana na Royalty au aajiri mfanyakazi wa kukaa na mtoto vinginevyo asiwe na haki ya kukaa naye.

Mama huyo pia anataka mahakama imfanyie vipimo vya dawa za kulevya Chris na imzuie kuvuta bangi kutumia pombe anapokuwa karibu ya Royalty.

Mbali na hivyo, Nia pia anataka aongezewe fedha za matunzo kutoka Dola za Kimarekani 2,500 hadi 16,000 kwa mwezi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.