Baada ya kupikwa akapikika, mshindi wa BSS 2015 Kayumba kuzindua video aliyoshoot S.A wiki hii. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya kupikwa akapikika, mshindi wa BSS 2015 Kayumba kuzindua video aliyoshoot S.A wiki hii.

Mshindi wa shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search 2015, Kayumba Juma kutambulishwa rasmi kama msanii weekend hii, kwa kuzindua video ya wimbo wake wa kwanza toka alipotangazwa mshindi wa shindano hilo mwaka jana.

Kupitia Instagram yake Kanyumba alishea habari njema na mashabiki.

“Asante #mungu kwa kuzifanya siku mbili hizi zilizo fatana kuwa ni siku za muhim kwangu Nikiwa na maana kwamba tarehe 5/2/2016 #mabirthday na tarehe 6/2/2016 kutakuwa na uzinduzi wa #Vidio yangu Utakao fanyika viwanja vya #mwembeyanga #MSIKOSE”

Kayumba ambaye yuko chini ya usimamizi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe cha Said Fella pamoja na uongozi wa BSS kwa sasa, ameshoot video Afrika Kusini wiki kadhaa zilizopita.
Kayumba akiwa na Justin Campos na Tale

Mwezi December 2015 Said Fella aliiambia Bongo5 kuwa Kayumba alisafiri na timu ya BSS kwenda Afrika Kusini kushoot video hiyo na director aliyefanya video ya Shaa ambaye ni Justin Campos wa Gorilla Films.

Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona kama uwezo mkubwa waliomuona nao Kayumba kwenye BSS utaweza kuendelezwa kwenye project zake binafsi, kitu kilichoshindikana kufanikiwa kwa baadhi ya washindi wa shindano hilo waliopita.

Hizi ni baadhi ya picha za BTS ya wakati wa utengenezwaji wa video hiyo”


video vixen wa video hiyo

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.